Aisha: Jike kutatiza pwani 2022

Usidanganyane, ndoto za magavana Hassan Joho wa Mombasa na mwenzake Amson King wa Kili?  kupigania Urais 2022 ni ombwe tupu kutokana na mjengo wa siasa nchini kugubikwa na wingu zito la naibu rais William Samoei Ruto.

Mkono wa mbabe wa Bonde la Ufa umeathiri mengi na wengi mkoani pwani msimu huu wa mageuzi-katiba na uchaguzi mkuu ujao. Ushahidi ni Aisha Jumwa mbunge wa Malindi kufungiwa milango mikuu ya Orange Democratic Movement (ODM) kwa kusuhubiana na Ruto kiasi cha kumnasia viongozi takribani 20 mkoani pwani. Hadi sasa athari za mkasa wa mama huyu mbishi zinaendelea na zitaendelea kuchafua mitazamo na hata wachini wao (ikiwemo wapiga kura) kaunti zote sita za pwani. Kuna kidonda chengine; utengano wa uhasama pwani.

Bado sijasahau Seneta Stewart Madzayo wa Kili?  alivyowakemea Joho na King waache kati kuzozania hadharani njozi za urais 2022 ilhali hawajaelewana nani kati yao atasimama kidete dhidi ya Rais Uhuru Keynatta, Raila Odinga, William Ruto, Kalonzo Musyoka, Gideon Moi, Fred Matiangi, Musalia Mudavadi na wengineo kutoka Bara wanaokodolea macho hatamu za ikulu 2022 na ? kra za wengi mkoani.

Wapwani wanashindwa wapi na vipi makungwi katikati ya vurumai la siasa na uongozi nchini wakati mkoa huu (tofauti na mikoa mengine nchini yenye vyama vya ”nyumbani”) bado unauguza makovu ya historia mbovu ya Shirikisho Party Of Kenya (SPK) ya Suleiman Rashid Shakombo na KADU ya Ronald Gidieo Ngala.

Mpwani kutawala Kenya kutawala Kenya kutokana na pupa, tamaa na ufuska wa maono ya viongozi. Ni hali ya uvundo ambayo imesambaa kabla na baada ya Uhuru wa Kenya 1963.

Kitendawili kikubwa Swali, ikiwa masimbari kama Sheikh Abdullah Nassir, Ngala na Shakombo walihodorora wakashindwa kupasua, sembuse Joho na Kingi wenye vibanda mwili na mirija midomoni kwenye angavu za mwambao. Haimkiniki kuwa wawili hao wataweza kuweza kukwepa ama kukatili mitego ya Baba Tinga na ? ni? nyange wazimu za siasa-dume za Kenya kutokana na upungufu wa pumzi, uchu na nyenzo asilia katika kupigania-(Wacha kushinda)- kura za urais 2022 ama siku za usoni.

Mafungu ya kisiasa Fungu hili la wasomi na wadadisi limebakishwa kuuliza na kujiuliza maswali chungu mbovu juu ya kitimtimu hiki cha magavana hawa bila kupata mtu ama taasisi ya kuwajibu huku likiendelea kupingwa na kundi dogo chini ya Amason Kingi mwenyewe. Kundi hili la pili linataka umoja wa pwani na wapwani kwanza kabla kuzungumzia ama kuzindua mshika bendera rasmi wa pwani.

Isitoshe wanapinga Joho kufanywa mteule kabla muungano wa pwani kuhusishwa. Wanateta; “shida yetu umoja; kwanza tuunganishe wapwani ndipo tuzungumzie nani atuongoze 2022. Gurupu ya tatu inataka Joho awe mwanambele haraka iwezekanavyo kama si sasa ni sasa hivi. Hapa kuna mbunge Teddy Mwambire(Ganze)na wenzake Abduswamad Sharrif Nassir(Mvita), Omar Mwinyi (Changwamwe), Ken Chonga (Kili?  Kusini), William Kamoti (Rabai) na Aisha Hussein mwakilishi wanawake na kaunti ya Mombasa.

Kundi la nne na mwisho ni waasi sugu wa vyama vyao (ikiwemo ODM) wanaochochewa na Aisha Jumwa, Mbunge wa Malindi. Hawa hawana haja wala ukaja na Joho kivyovyote; watakalo ni naibu Rais William Ruto kumrithi rais Uhuru Kenyatta 2022, wapende wasipende. Wanajiita MV. HATUSHUKI na sielewi watakuwa wageni wa nani iwapo Ruto atashukishwa mbele ya safari.

Nauliza: Nini mbaya na Sultan Joho na Kubo Amason Kingi mpaka watu? kishe hapa? Mbona wagawanye wapwani kabla kura ya maoni na uchunguzi mkuu ujao? Je, wanajifurahisha tu ama wamedindia kupendua na hisia za wapwani zilingane na hawa-nafsi zao bila kujali mazingara na maamuzi yao? Je, wapwani wana laana ya kutoungana? Njia panda Madhambidhambina wa siasa mkoani pwani wanapakazia Amason Kingi kama subiani anaezunguka nje ya kasri la William Ruto bila ya kuingia ndani, mlango ni samba jike Aisha Jumwa akaishiria sebuleni.

Je, Kubo huyo wa Kili?  atabwaga nyatiti na gushe ajitose ndani kwenye mkuki wa kinandi ama atabakia kuzurura nje ya kasri la naibu rais? Mkong’oto baina Raila na Ruto uko pwani-mdomo wa Kenya na nchi za maziwa makuu. Jumwa ni tanuri la tishio kwa Joho na itakuwa kazi pevu kumzima.

Ruto anahitaji Jumwa awe fahali wa pili dhidi ya Sultan wa Mombasa ili kuwapa wapwani mlango mwengine wa kupitia wa? kie Kanani. Jambo jengine :kuna chembe cha uhasama wa kikabila baina ya Joho na akina Jumwa na Kingi ambao ni wa jamii ya Giriama. Kufukuzwa kwa

Jumwa ODM ilhali mwenzake Suleiman Dori (mbunge wa Msambweni na mswahili kama Joho) akaponea huku kumeleta chuki na ? tna za wenyeji wa Kili?  na jamii ya Kigiriama sehemu ya Kisauni na kwengineko sehemu ya kaunti ya Mombasa. Jumwa na Dori wote walikua msitari wa mbele kumpigia debe RUTO alipofanya kali kuteka wabunge 20 wa Pwani- jambo lililomuudhi Raila, Joho na maa? sa wa ODM.

Siajabu Kingi kulalamika mkutanoni shule  ya msingi ya Mtomondoni hivi majuzi akiwauliza Joho na viongozi wengine: “Itakuwaje niwe mwana mbele wa Pwani kupigania urais 2022 iwapo Kili?  inaelekea huku, Mombasa yaelekea kule nayo Lamu, Tana River na Taita Taveta zinaelekea kwengineko? Je nitakua naongoza Kili?  ama eneo la Pwani?” Kitendo cha Joho kujipiga kifua hadharani mnamo Machi 25 mwaka huu kuwa ndiye bora wa Pwani kupigania uraisi bila shaka ni tendo la kiburi na ubwana machoni na masikioni mwa akina Kingi na wenyeji wa Kili?.

Isitoshe, Joho ameudhi jamii hio kwa kuamua kusimama nyuma ya Najib Balala na Abdulswamad Nassir (mbunge wa Mvita)  bila kumsahau spika wa bunge la Mombasa Arub Khatri kama warithi bora wa Gavana huyo 2022 kulikoni Naibu Gavana Dkt. Wiliam Kingi na katibu wake Francis Thoya ambao wote ni wenyeji wa Kili? .

Jumwa atavalia gwanda la jike dume la pwani?

Akikoroga sauti yake nje ya nyumba kama hujapata kumsikia ama kumuona maishani mwako, utamdhania ni dume laleleja maneno hapo. Wale waliomuona na kukurubana naye wakati wa uchaguzi mdogo wa Malindi, mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa 2017, wanakubaliana nami kwamba bila kujali, alipigana mieleka na baadhi ya wabunge fulani wa Jubilee ambao alidai walikuwa wananunua kura siku hiyo ya uchaguzi mdogo.

Leo hii, ukimwuliza gavana wa Kiambu, Ferdinand Waititu bila shaka atakuambia ni ukweli kwani hata yeye alikurubana naye wakati wa uchaguzi mdogo wa Malindi. Je, wajua ni kwa sababu gani viongozi wengi wa chama cha ODM, akiwepo kinara wake Raila Odinga anafuatilia mambo yake mosi mosi na wengine kuongelea bafuni? Jibu li wazi kuwa mdomo wa Aisha Jumwa daima uko wazi na unaweza kutapiga hata matapishi yasiyozoleka ya kisiasa. Maana ya kuitwa “Jike Dume” toka wakati akiwa mwakilishi wa kina mama wa Kili?  (2013-2017), ni kwa sababu ya ushujaa wake. Muulize aliyekuwa waziri msaidizi na mbunge wa Ganze Francis Baya, atakuambia zaidi.

Waulize wananchi wote wa kaunti ya Kili? , kina mama wote ambao wakati mmoja walikuwa wakishikwa na mzizimo wa hofu mikutanoni ambapo bila ya kuwaogopa, alikuwa anawaambia wenzake, wakilegezea mabwana wao, yeye atapita nao. Uliza wale ambao walibishana naye, watakuambia kwamba mdomo wa Aisha Jumwa unatoa nyoka pangoni na pia unaweza kutongea kichwa kugotwa.

Kwa kuwa mwaka 2022, magavana Joho na Kingi watakuwa hawana msukumo mkubwa wa kutafuta vyeo vyovyote vile vya jimbo, Jumwa huenda akawa moto wa kuotea mbali kwa wale atakaowaunga mkono na akawa sumu kwa wale anaopingana nao.

Credit: Source link